HISTORIA YA CHAMA CHA REPUBLICAN ENZI ZITANGULIAZO VITA VYA WENYEWE KWA WENYEWE MAREKANI

SAHAU NI DAWA YA MJA

Mengi yameandikwa juu ya mchango wa chama cha Republican kukomesha utumwa Marekani. Yanayo fichwa ni sababu zilizosukuma wanachama wengi kufanya hivyo.  Madhumuni ya makala hii ni kueleza msimamo wa waliowengi wanachama wa chama hicho kuhusu haki ya kumfanya binadamu mali ya mtu.

Tuanzie na uchunguzi wa jina rasmi ya taifa linalojulikana kama “Marekani”.  Jina hili tafsiri yake kwa Kiswahili ni: Umoja wa Majimbo ya Marekani.  Katika Kiingereza ni: The United States of America.  Neno jimbo lina maana tofauti sana katika Kiingereza ikilinganishwa na maana yake katika Kiswahili.  “Jimbo” au “state” ni ya pili katika miundombinu ya kisiasa kuanzia na serikali kuu yaani serikali ya taifa zima inayoongozwa na rais halafu kuwa na serikali ya kila jimbo inayoongozwa na gavana.

Kila jimbo katika enzi zilizotangulia vita vya wenyewe kwa wenyewe lilijipitishia sheria kukubali utumwa au kuupiga marufuku. Majimbo karibu yote ya sehemu za kaskazini Marekani ambako uchumi wa viwanda ulikuwa unaongoza yalipiga marufuku utumwa.  Majimbo ya sehemu za kusini Marekani ambako uchumi ulikuwa wa kulima kwa pamba na tumbako kwa ujumla yalitegemea unyonyaji wa watumwa katika mashamba makubwa.   Nayo yale makubwa yalimilikiwa na asilimia moja tu ya watu huru kwa maana watu tajiri walikuwa asilimia moja ya watu huru wote wa majimbo ya kusini.  Kiwango cha pili ni wale waliokuwa na angalau mtumwa mmoja huenda wachache nao walikuwa asilimia theluthi moja ya watu huru.  Jambo linalosisitizwa ni asilimia theluthi mbili ya watu huru wengi wao walikuwa maskini hawana ardhi nzuri wala kazi ya kudumu.  Kazi za kibarua zenye hatari mno ziliajiri wazungu maskini watumwa wakilindwa kwa sababu ya thamani yao katika uchumi wa kila jimbo la sehemu za kusini MarekanI.

Chama cha Republican kilikuwa chama cha waliowengi wa majimbo ya kaskazini huku chama cha Democratic kilikuwa kinapata kura za waliowengi wa majimbo ya kusini.  Dhamira ya makala hii ni kueleza sababu za chama cha Republican kuchukia utumwa kwa vile utumwa haukuwepo katika majimbo mengi ya kaskazini.  Suala hili kiini chake ni la kiuchumi mbali na suala la haki ya binadamu.  Chama cha Republican kiligawanyika katika vikundi vitatu, cha kwanza katika ukubwa kiliitwa kwa Kiingereza “Unionists”.  Tafsiri yangu ya jina la kikundi hicho ni “la kwanza ni umoja wa majimbo yaani umoja wa taifa, halafu”.  Cha pili katika ukubwa kiliitwa “Free Soilers”  maana yake ni kinyume na maana tegemea ya jina hilo.

Maana kusudia ilikuwa kutambulisha ardhi inayopiga marufuku watu wote ila Wazungu nao ndio wenye asili ya Uingereza na Ujerumani pamoja na wale wa Skandinavia.  Walichukia kuwepo Marekani kwa Waireland  na Waitalia.  Porojo ya kikundi hichi ilisisitiza ya kuwa Waireland na Waitalia waliohamia Marekani wameshapora kazi za Wamarekani wa kweli.  Endapo idadi ya watumwa itazidi idadi inayohitajika katika kulima eneo la ardhi linalolimika katika majimbo ya kusini, mabeopari wenye viwanda vilivyoko sehemu za kaskazini watawaleta watumwa wale ziada wawe wafanya kazi wanyongwe hali ajira ya Wazungu, Wamarekani wa kweli itapunguka zaidi.  Wafanya kazi walihamisishwa kupigania vita kukanusha utumwa ili wasije kunyang’anywa ajira.  Walisisitiziwa ya kuwa utumwa unaokoa Mwafrika kutoka katika hali ya njaa, maradhi na ushenzi wa Afrika.  Isipokuwa utumwa wake Mwafrika hawezi kumudu Marekani.  Tukiwaachilia huru, wote watakufa na njaa.  Hakuna haja kuwabagua waachilie kujitegemea watapondana wenyewe kwa wenyewe ushenzi utawakumbatia njaa ndiyo itakuwa lishe yao.

Kundi la tatu liliitwa “Abolitionists” yaani watu ambao waliona utumwa kuwa ni dhambi walioamini binadamu wote ni sawa.  Kundi hili ndilo hutangazwa na kufundishiwa shuleni zaidi marudufu kuliko kundi la “Free Soilers”.  Lakini kundi hili lilikuwa dogo sana!  Kundi hilo peke yake liliwakaribisha watu wote kuishi popote wapendapo Marekani.  Kundi hilo peke yake lilisisitiza haki ya mtu yeyote mwenye heshima zake kuwa raia wa Marekani.

Kukirudia kundi la kwanza, “Unionists”  mtu mashuhuri katika kundi hilo alikuwa Marehemu Mheshimiwa Rais Abraham Lincoln.  Naye alisema kuhusu utumwa:  “Kipaumbele changu ni kuhifadhi na kuulinda umoja wa majimbo ya taifa la Marekani. Nchi ya Marekani inakubali taifa moja tu!  Kama naweza kutekeleza lengo hili huku utumwa nao ukiendelea, utumwa uendelee.  Endapo utumwa unagawa majimbo na mengine yatangaze  azimio la taifa jingine likiwa na serikali kuu yake, tutakanusha utumwa.

Matokeo ya kutengana baina ya wawakilishi wa majimbo katika serikali kuu yakawa vita vya wenyewe kwa wenyewe na kutangazwa kwa azimio la kuwaachilia huru watumwa waliokuwepo majimboni mwa Confederate States of America, ndilo jina la taifa jipya lililojitenga na United States of America.  Jina la azimio hilo katika Kiingereza ni “Emancipation Proclamation”.  Baada ya majeshi ya serikali kuu ya United States of America kushinda majeshi ya serikali ya “Confederate States of America”, rekebisho la kumi na tatu la Katiba ya Umoja wa Majimbo ya Marekani lilipitishwa nalo likakanusha utumwa kisheria  katika majimbo yote ya Marekani; nchi nzima.

Pete Mhunzi

Profesa Mstaafu wa Historia

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s