SHULE BORA 20 za SERIKALI 2013

Na Abeid Poyo, Mwananchi

KWA UFUPI

  • Uchambuzi huu umezingatia kigezo cha shule kongwe kihistoria. Ni zile zilizoanza kabla ya uhuru.

Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne yaliyotoka hivi karibuni yanaweza kutazamwa kwa sura mbalimbali.  Kwa mfano, baadhi ya wadau wa elimu wanasema kwa mazingira yalivyo kati ya shule binafsi na zile za Serikali, si busara kuzilinganisha kimatokeo.

Wadau hawa wanatoa mifano ya tofauti kubwa iliyopo ya mazingira ya ufundishaji na ya kujifunzia baina ya shule hizo.  Mifano wanayotoa ni pamoja na uhaba wa walimu na vifaa vya kujifunzia uliotamalaki katika shule nyingi za umma. Hivi wanasema ni miongoni mwa vichocheo muhimu vinavyoimarisha taaluma shuleni.

Katika makala haya, mwandishi amechambua matokeo kwa minajili ya kubaini shule zilizofanya vizuri, kwa kutazama kigezo cha shule za Serikali hususan zile kongwe zilizotamba kwa kiwango kikubwa miaka ya nyuma.  Uchambuzi huu unahusisha shule 20 bora kwa kuangalia madaraja waliyopata wanafunzi na nafasi ya shule katika orodha ya shule bora kitaifa.

Sekondari ya Mzumbe

Imeshika nafasi ya 40 kitaifa. Ufaulu kwa madaraja ni kama ifuatavyo: daraja la kwanza (57), daraja la pili, (27), daraja la tatu (15), daraja la nne (9). Hakuna daraja sifuri

Sekondari ya Ilboru

Imeshika nafasi ya 41 kitaifa. Daraja la kwanza (55), daraja la pili, (21), daraja la tatu (23), daraja la nne (5). Hakuna daraja sifuri

Sekondari ya Kibaha

Imeshika nafasi ya 44 kitaifa. Daraja la kwanza (44), daraja la pili, (31), daraja la tatu (12), daraja la nne (9). Hakuna daraja sifuri

Sekondari ya Lumumba

Imeshika nafasi ya 51 kitaifa. Daraja la kwanza (10), daraja la pili, (10), daraja la tatu (1), daraja la nne (2). Hakuna daraja sifuri

Sekondari ya Wavulana Tabora

Imeshika nafasi ya 56 kitaifa. Daraja la kwanza (42), daraja la pili, (20), daraja la tatu (9), daraja la nne (13). Hakuna daraja sifuri

Sekondari ya Kilakala

Imeshika nafasi ya 62 kitaifa. Daraja la kwanza (34), daraja la pili, (32), daraja la tatu (7), daraja la nne (10). Hakuna daraja sifuri

Sekondari ya Msalato

Imeshika nafasi ya 65 kitaifa. Daraja la kwanza (29), daraja la pili, (32), daraja la tatu (24), daraja la nne (2). Hakuna daraja sifuri.

Sekondari ya Fidel Castro

Imeshika nafasi ya 83 kitaifa. Daraja la kwanza (29), daraja la pili (32), daraja la tatu (24), daraja la nne (2). Hakuna daraja sifuri.

Sekondari ya Wasichana Tabora

Imeshika nafasi ya 147 kitaifa. Daraja la kwanza (15), daraja la pili, (20), daraja la tatu (21), daraja la nne (17), daraja sifuri (2).

Malangali Sekondari

Imeshika nafasi ya 172 kitaifa. Daraja la kwanza (7), daraja la pili, (26), daraja la tatu (16), daraja la nne (2), daraja sifuri (6).

Sekondari ya Ifunda

Imeshika nafasi ya 205 kitaifa. Daraja la kwanza (24), daraja la pili (40), daraja la tatu (18), daraja la nne (22), daraja sifuri (14).

Sekondari ya Jangwani

Imeshika nafasi ya 226 kitaifa. Daraja la kwanza (40), daraja la pili (71), daraja la tatu (52), daraja la nne (67), daraja sifuri (35).

Sekondari ya Wasichana ya Iringa

Imeshika nafasi ya 241 kitaifa. Daraja la kwanza (15), daraja la pili, (28), daraja la tatu (15), daraja la nne (27), daraja sifuri (18).

Sekondari ya Wavulana Bwiru

Imeshika nafasi ya 242 kitaifa. Daraja la kwanza (20), daraja la pili (18), daraja la tatu (13), daraja la nne (32), daraja sifuri (12).

Sekondari ya Wavulana Songea

Imeshika nafasi ya 257 kitaifa. Daraja la kwanza (12), daraja la pili (10), daraja la tatu (14), daraja la nne (17), daraja sifuri (8).

Sekondari ya Zanaki

Imeshika nafasi ya 276 kitaifa. Daraja la kwanza (13), daraja la pili (60), daraja la tatu (66), daraja la nne (63), daraja sifuri (26).

Sekondari ya Kantalamba

Imeshika nafasi ya 310 kitaifa. Daraja la kwanza (15), daraja la pili (29), daraja la tatu (48)daraja la nne (34), daraja sifuri (37).

Sekondari ya Pugu

Imeshika nafasi ya 325 kitaifa. Daraja la kwanza (14), daraja la pili (16), daraja la tatu (22)daraja la nne (36), daraja sifuri (16).

Sekondari ya Azania

Imeshika nafasi ya 333 kitaifa. Daraja la kwanza (54), daraja la pili, (67), daraja la tatu (96)daraja la nne (121), daraja sifuri (87).

Sekondari ya Kibasila

Imeshika nafasi ya 337 kitaifa. Daraja la kwanza (32), daraja la pili (89), daraja la tatu (90)daraja la nne (129), daraja sifuri (89).

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s