TUTUMIE HII SANAA KU . . .

MAIMUNA KUBEGEYA

TUTUMIE HII SANAA KUITANGAZA NCHI YETU

Awali alikuwa akitegemea kuuza bidhaa zake kwenye duka lake lililokuwepo maeneo ya Moroco jijini Dar es salaam. Akiwa hapo aliweza kupiga hatua zaidi na hata kushiriki maonyesho ya mitindo, akilenga kuonyesha ubunifu wake.PICHA|MAKTABA 

Na Maimuna Kubegeya, Mwananchi

Posted  Jumapili, March 29  2014  saa 11:12 AM

KWA UFUPI

“Kadri siku zilivyokuwa zikienda nikawa napata uzoefu wa kuhudhuria matamasha mengine hadi kufikia mwaka 2009, niliposimama na kufanya onyesho la peke yangu.

“Naweza kusema sanaa inachukua muda mwingi wa maisha yangu. Kwani katika kila dakika ninayoishi, nimekuwa nikiitumia kufikiri ni kitu gani kipya cha ubunifu naweza kufanya kujiingizia kipato,” anaanza kusema mbunifu wa mitindo na msanii wa mkongwe nchini Fatma Amour.

Fatma Amour anayemiliki pia Kampuni ya Famour alianza rasmi kazi hii ya ubunifu wa mavazi na kazi za mikono mwishoni mwa miaka ya 90, akiwa miongoni mwa wabunifu machachari wa kike waliokuwa wakifanya vizuri zaidi wakati ule.

Akiwa miongoni wa waanzilishi wa Taasisi ya Tanzania Mitindo House ya jijini Dar es Salaam, Fatma amekuwa mstari wa mbele katika kubuni mavazi yanayoendana na utamaduni wa Kiafrika.

“Ukiachilia mbali mambo ya ubunifu wa mitindo, nimekuwa nikibuni mapambo mbalimbali nikitumia malighafi zinazopatikana ndani ya nchi,” anasema.

Anasema pia ubunifu wake hutegemea oda anazopata kutoka kwa wateja, wakati mwingine hulazimika kuagiza malighafi kutoka nje ya nchi.

Baadhi ya bidhaa zinazotengenezwa na mbunifu huyu ni zile zinazotokana na malighafi ya ngozi, kama vile viatu, mikoba, mapambo kwa ajili ya ndani na mazulia ya ngozi. Nyingine ni hereni, magauni na mavazi mengine.

Awali alikuwa akitegemea kuuza bidhaa zake kwenye duka lake lililokuwepo maeneo ya Moroco jijini Dar es salaam. Akiwa hapo aliweza kupiga hatua zaidi na hata kushiriki maonyesho ya mitindo, akilenga kuonyesha ubunifu wake.

Kwa wakati huo aliweza kushiriki kwenye maonyesho ya mitindo, yakiwemo Swahili Fashion Week, Kanga ya kale na Lady in Red .

“Kadri siku zilivyokuwa zikienda nikawa napata uzoefu wa kuhudhuria matamasha mengine hadi kufikia mwaka 2009, niliposimama na kufanya onyesho la peke yangu.

“Onyesho hilo lilijulikana kwa jina la Kakakuona. Nilitoa moja ya matoleo yangu. Tofauti na matoleo mengine, toleo hili lilikuwa limesheheni mavazi ya ngozi,” anasema.

Baada ya kujihusisha zaidi na ubunifu wa mavazi, aliona ipo haja ya kupanua wigo akilenga kutengeneza bidhaa nyingi zaidi zitakazomwingizia kipato.

Akiwa kwenye mpango huo, aliona ipo haja ya kujiunga na wabunifu wenzake kwa kufanya maonyesho ya bidhaa zake pamoja na kujiunga na vikundi vya wajasiriamali wanaotengeneza bidhaa za mikono.

Kujiunga kwake huko kulimwezesha kupata fursa ya kuhudhuria maonyesho mbalimbali ya kazi za mikono, ndani na nje ya nchi.

“Nimekuwa nikiuza bidhaa zangu katika maonyesho ya kibiashara yanayofanyika nchini. Miongoni mwa maonyesho hayo ni pamoja na yale ya Saba Saba na mengine ya wajasiriamali yanayofanyika kila mara,” anasema.

Uamuzi wake wa kujikita kwenye utengenezaji wa kazi hizo ulimwezesha kupata fursa ya kushiriki maonyesho mengine ya kimataifa katika nchi mbalimbali za Afrika.

“Baadhi ya nchi nilizowahi kutembelea ni nchi zote za Afrika Mashariki, Zambia, Malawi, Botswana, Afrika Kusini, Msumbiji, Ethiopia na Zimbabwe,” anasema.

Akizungumzia hali halisi ya ubunifu iliyopo baina ya nchi alizotembelea na Tanzania, anasema kuna tofauti kubwa kwa baadhi ya nchi.

Katika nchi zote za Afrika. Afrika Kusini wako juu zaidi kiubunifu tofauti na nchi nyingine. Wengine wengi naweza kusema tunawazidi na wengine tupo sawa.

Kuna nchi mbili anazodai kuwa zinaweza kuwa tishio katika suala zima la ubunifu. Nchi hizo ni Uganda na Rwanda. Kwani hawa tofauti na wengine wao wamejikita katika kuhakikisha wanaboresha utamaduni wao.

Mara nyingi hata wanapokuja kwenye maonyesho ya kimataifa, kikubwa wanachozingatia ni kuhakikisha wanauza bidhaa zenye asili ya utamaduni wao.

Jambo hili lingetakiwa kuigwa hata na wabunifu na wasanii wa Kitanzania. Ikiwa wataelekeza nguvu zao katika kutengeneza bidhaa zenye asili yetu, ni wazi kuwa kutakuwa na upekee wa bidhaa zetu.

Tofauti na ilivyo sasa. Watanzania wengi wameshindwa kuwa na ubunifu katika suala zima la utengenezaji wa bidhaa. Kwani hakuna anayetaka kutengeneza bidhaa ya asili. Wengi wamejikita katika kuiga bidhaa za watu wa nchi nyingine.

“Kwa mtazamo wangu mambo kama haya yanaua siyo tu ubunifu wa asili, bali pia uwezo wa mbunifu mmoja, mmoja wa kubuni bidhaa zitakazoweza kuingia na kushindana kwenye soko.

“Wakati umefika kwa wabunifu wa kitanzania kujifunza kutoka kwa wenzetu. Kusimama pamoja na kutengeneza bidhaa zenye asili ya Kitanzania ndiyo njia pekee ya kuipa hadhi nchi yetu kupitia kazi zetu” anasisitiza.

Kikubwa kinachotakiwa ni kuchangamkia fursa zote zinazojitokeza hususani zile za kujiendeleza. Wajasiriamali wasisite kujifunza msuala mbalimbali yatakayosaidia kufanya maboresho ya kazi zao anasisitiza.

Akizungumzia mipango yake ya baadaye, Fatma anasema ana mpango wa kusambaza ujuzi wake kwa watu wengine, hususani vijana wadogo.

“Kwa kuwa nina uzoefu mkubwa katika masuala ya utengenezaji na uuzaji wa bidhaa za kazi za mikono, mpango pekee nilio nao ni kuanzisha chuo cha mafunzo ya sanaa za kazi hizi za mikono”.

Advertisements

One thought on “TUTUMIE HII SANAA KU . . .

  1. Pius

    Nami ningependa kujikita kwenye sanaa kama Fatma, so ningefurah zaid kama naweza kupata mawasiliano yake nikafika ofisin kwake nijifunze mengi.

    Reply

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s