MATATIZO ya WANAFUNZI SI LUGHA MBILI

MATATIZO ya WANAFUNZI SI LUGHA MBILI NI KUTOSOMA LUGHA YOYOTE

na Pete Mhunzi                                                                                                                           Mhariri Mkuu

Leo katika toleo la pili la MSIMAMO ninaomba fursa ya kutoa ufafanuzi wangu  juu ya suala la lugha ipi inafaa Tanzania kuendeleza elimu, biashara, utaalamu  na utamaduni.

Ni nia yangu kutetea matumizi ya lugha zote mbili za Kiswahili pamoja na Kiingereza Tanzania.  Kiingereza kikiwa lugha ya kuwasiliana na dunia huku Kiswahili kikiwa lugha ya uzalendo katika Tanzania kwanza halafu huenda Afrika nzima.

Katika kusoma kwangu kwa magazeti ya Kitanzania pamoja na maoni yanayosikika katika mazungumzo baina yangu na Watanzania, Kiingereza kinapendezwa kuliko Kiswahili kutokana na matumizi yake dunia nzima.  Isitoshe istilahi zake za fani za sayansi, ujenzi na utaalamu ambazo Kiswahili kiko njiani kuzitunga.

Ni kweli, Kiswahili kinajengeka.  Kiingereza kilianza kujengeka katika ufalme wa Henry VIII katika karne ya kumi na tano.  Ndiyo sababu istilahi za Kiingereza za tiba na sayansi bado ni Kilatina si Kiingereza!   Ukoloni ulisambaza matumizi ya Kiingereza.  Ukoloni ulileta Kiingereza kwa bara la Marekani kama kilivyoletwa bara la Afrika.

Kama kichwa kinachosema matatizo ya wanafunzi Tanzania si Kiswahili badala ya Kiingereza.  Nionavyo mimi tatizo ni kutazama runinga pamoja na kuitumia simu ya kiganjani kuwasiliana katika maandiko ya lugha duni.

Huku Marekani hakuna lugha inayoshindana na Kiingereza.  Kiiingereza ni lugha rasmi katika shule, serikali, na vyuo vikuu.  Je, mbona asilimia ya wanafunzi wa shule za upili wanaoweza kusoma kulingana na kidato walio nacho ni kumi na mbili tu?   Jibu langu ni asilimia ile ya themanini na nane badala ya kusoma vitabu na magazeti  wao hutazama runinga pamoja na kutumia simu za kiganjani  kuwasilisha ujumbe za maandiko ambao lugha inayotumika nao ni duni.

Mimi ni profesa mstaafu.  Hebu turejee enzi za elfu mia tisa na sabini pamoja na themanini wanafunzi wageni walipoanza kuja Marekani kwa wingi kusoma chuo kikuu.  Siku ya kwanza katika muhula mara yangu ya kwanza kuonana na wanafunzi ningewaona wanafunzi wageni wakiwa na uwezo wa kusoma na kuandika Kiingereza kuwashinda asilimia kubwa ya Wamarekani wazaliwa.

Siku hizi hakuna tofauti.  Karibu wote Wamarekani kwa wageni  hawasomi, hawaandiki licha ya dhuluma ya kuwa Wamarekani hawafahamu shida yao kwa sababu wanaongea mambo ya kila siku pasi na matatizo mpaka matakwa ya ajira yanawakabidhi.   Hawafahamu  ya kuwa wamepata alama isiyostahiki katika madarasa ya Kiingereza, historia, siasa, na khadalika.

Maendeleo ya kiuchumi Tanzania na kwingineko yameleta runinga na vitu vingine vya kiteknologia ambavyo vinadunisha matumizi ya akili ya watoto na vijana huku wenyewe hawafahamu wanaenda kombo kwa sababu wanaongea lugha mtaani katika rika waliyo nayo wakiwapa kisogo wazazi pamoja na wazee.

Mapendekezo yangu mimi ni kutunza tabia ya kusoma.  Kusoma vitabu, magazeti, majarida na khadalika katika lugha mbili, Kiswahili pamoja na Kiingereza.

Ujenzi wa Kiswahili ni sehemu ya utu ambayo Tanzania peke yake imeshaanza kukamiliza.  Watanzania wote hawana budi kufahamu uongozi wa Marehemu , Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mheshimiwa Mwalimu Julius Kambaraje Nyerere.  Hakuna mtu siku hizi popote duniani anayeweza kumshinda katika ubobezi wa Kiingereza.  Hakuna mtu Afrika ya Mashariki anayejitahidi zaidi kujifunza na kukiendeleza Kiswahili.

Hayo ndio maoni yangu juu ya suala la lugha Tanzania.

Asanteni

Advertisements

One thought on “MATATIZO ya WANAFUNZI SI LUGHA MBILI

  1. Kitoto

    Hakuna suala muhimu kama kusoma vitabu, kusoma kwa jumla. Chimbuko la kutoelewa mambo, kujidharau kiutamaduni, kukimbilia vya wengine kiulimbukeni, kuharibu lugha kwa kudumisha “Kiswanglish”, ni kutokusoma. Na hiki “Kiswahnglish” kinadumishwa pia na baadhi ya viongozi au waheshimiwa wanaodhani kuweka maneno mawili matatu ya Kiing katika Kiswahili ni kujua. Afadhali wengi wao wamesoma. Wanaowaiga wengi wana elimu haba…
    Makala hii imegusa hilo na yabidi kusomwa hasa na vijana. Nimeupenda pia mstari unaosema kizazi kipya chastahili kujifunza toka kwa wazee. Kitakwimu idadi ya vijana ni kubwa kuliko wazee Tanzania leo. Hii ni kutokana na maradhi hasa UKIMWI na Malarua yaliyowamaliza raia wengi wa makamo. Maendeleo si simu za mkononi, teknolojia au kusema maneno mawili matatu ya Kiingereza. Maendeleo ni kupenda ulicho nacho: lugha, desturi, ardhi, vyakula, nk…

    Reply

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s