HISTORIA YA UBAGUZI MAREKANI

_MG_0012Na Pete Mhunzi

Asili yake si Afrika wala rangi ya ngozi asili ndiyo dini ya Kanisa la Uingereza

Makala hii inafuata makala iliyopo blog hii iitwayo “Hate Without End.” Madhumuni yangu ni kuongezea vipengele vilivyopo na kusisitiza hoja zinazoeleza kwa kina historia ya ubaguzi Marekani nikiwa na nia ya kuonyesha ya kuwa ubaguzi ulikuwepo Marekani kabla ya uvamizi wa Afrika na matokeo ya uvamizi huo yakawa ukoloni na utumwa ambayo yalianzia Uingereza. Taifa la Marekani likaumbika kutokana na kuungana kwa makoloni ya Uingereza, pamoja yakapigania uhuru na kuwa taifa liitwalo Umoja wa Majimbo ya Marekani. Kila jimbo lilikuwa koloni kwanza.
Dhamira ya makala hii ni kueleza asili ya ubaguzi Uingereza na jinsi ulivyoenda Marekani katika madhehebu ya walowezi. Sababu za ubaguzi zinatokea katika dini ya Kanisa la Uingereza ikiwa pamoja na madhehebu mengine yaliyosambaratika baada ya Kanisa la Uingereza kuasisiwa kutokana na kujitenga kwa Uingereza na Kanisa Katoliki. Makanisa hayo yote yakiwa na Kanisa la Uingereza yanajumlishwa katika jina la Maprotestanti. Miongoni mwao ni pamoja na makanisa ya Kilutheri, Kikuweka, Kipuritani, Kibaptisti, Kisabato, kanisa la Presbiteri, kanisa la Pentikosti, Jamii ya Marafiki na kadhalika.
Waingereza waliokuja Marekani walikuwa kwanza waamini wa madhehebu hayo ambao walikataa kuwa waamini wa Kanisa la Uingereza ijapokuwa waliungana na kanisa la Uingereza katika kubagua Wakatoliki. Wao wote pia walibaguliwa na serikali pamoja na Kanisa la Uingereza na ndiyo sababu wakaamua kwenda Marekani wakawa walowezi wa kwanza katika Marekani ya Kaskazini.
Enzi za Mfalme Henry VIII wa Uingereza ndizo zilizoleta mgogoro baina ya Ufalme wa Uingereza na Kanisa Katoliki. Yeye Mfalme Henry aliomba talaka kwa vile mke wake hakuzaa mtoto wa kiume na akakatazwa na Kanisa Katoliki. Naye Mfalme Henry akaamua kujitoa kutoka katika Kanisa hilo akiongoza Ufalme wa Uingereza kujitoa vile vile kisha Kanisa la Uingereza likaanzishwa likiwa na nia kuwabadilishia dini Waingereza Wakatoliki wote wawe waabudu wa dini mpya ya Kanisa la Uingereza.
Pamoja na mabadiliko ya dini yalitokea mabadiliko ya lugha ndipo Kiingereza kikawa lugha rasmi ya Uingereza huku lugha ya Kilatini ikabaki kueleza sayansi. Kutokana na uamuzi huo hatimaye lugha zote zilizokuwa lugha sokoni Ulaya zisizo na hadhi zikiwa lugha za watu masikini Ulaya zikawa lugha rasmi za mataifa ya Ulaya hata yale yaliyoendelea kuabudu dini ya Kikatoliki, mifano ni Ufaransa, Hispania, Italia na mataifa ya Ulaya wa Mashariki. Kabla la mabadiliko ya lugha Ulaya, Kilatini kilikuwa lugha iliyounganisha falme zote za Ulaya katika Kanisa Katoliki ikiwa lugha ya dini, elimu, na lugha mama ya matajiri wote.
Mfano nyeti wa porojo ya Uingereza ulikuwa kusema Wakatoliki wote wanaona Papa Baba Mtakatifu, kuwa mfalme wa Wakatoliki wote huku serikali zote za mataifa yao yapo chini ya utawala wake. Porojo hiyo iliendelea kuwatambua Waingereza kuwa watu ambao wanajitegemea kuliko kuwa wafuasi wasio na haki. Nao wanaheshimu serikali lakini hawaogopi serikali. Wanaheshimu mfalme hawaabudu mfalme.
Mfano mwingine muhimu wa ubaguzi wa Uingereza dhidi ya Kanisa Katoliki unatokea katika Mahakama ya Kanisa Katoliki ya kukomesha uasi karne ya 15 na 16. Baada ya serikali ya Hispania kufukuza Waislamu kutoka katika Hispania wakiwa watawala wa sehemu za kusini Hispania, mahakama hayo yalidhulumu watu wote wasio Wakatoliki kuwa washenzi ambao wamebarikiwa na fursa ya kuabudu dini ya Kikatoliki wakaribishwe katika Ufalme wa Mungu. La sivyo wengine walichomwa moto wangali hai. Waislamu kutoka Afrika Magharibi walikuwa wanatawala sehemu za kusini kwa Hispania pasi na kuwabagua wengine ambao walikuwa waabudu wa dini nyingine mfano ni Wayahudi.
Kanisa la Uingereza kama kanisa la Katoliki lilitaka Waingereza wote waabudu dini ya Kanisa la Uingereza lakini wale waliokataa walipewa fursa ya kwenda Marekani wawe walowezi badala ya kuuawa. Wakiwa Marekani wangeendelea kunufaisha Uingereza mradi hawaishi Uingereza. Kutokana na maadili haya nadharia ya ubeopari ukachangiwa ukiwa na kipengele kinachokazia ya kwamba kunyonga watu ni bora kuliko kuwaua watu kwa vile maiti haina thamani kiuchumi hakuna maslahi kwa nchi tawala katika kuwaua watu wasio na heshimu hata washenzi.
Porojo la Uingereza ulisisitiza thamani ya binadamu kiuchumi. Hata mshenzi unakadiriwa kiuchumi katika dini ya Kanisa la Uingereza huku Kanisa Katoliki unasisitiza unyenyekevu wa dini kwanza halafu wa wale wa tabaka la juu hasa wale wenye kasumba za kimwinyi. Porojo ilitambulisha Wakatoliki watu wenye hulka zilizo na msingi wa hisia mbali na msingi wa matumizi ya akili na busara yanayonufaisha wananchi wa nchi husika. Hata akili za watu masikini zinastahili kutumika ilimradi changamoto iwe baina ya wasomi pamoja na wataalamu wakipashana habari na watu masikini badala ya ngome ya maringo ya watu wa tabaka la juu wanaowadharau watu masikini.
Hatimaye mapinduzi ya viwanda yalitokea katika Uingereza, Ufaransa, Marekani, na Ujerumani. Nchi nne, na tatu katika nchi hizo nne zikiwa na serikali zisizo na utawala wa Kikatoliki. Sasa porojo ikasisitiza waabudu wa dini ya Kikatoliki hawajui thamani ya kazi, hawajui kuongoza jamii, wanatawaliwa na hisia siyo busara na hawawezi kushindana nasi Waprotestani.
Mfano wa mwisho katika utangulizi wa maelezo ya ubaguzi Marekani ni mgogoro baina ya Ireland na Uingereza. Msingi wa mgogoro ni dini ya Kanisa Katoliki.
Marekani kulikuwa na makoloni kumi na matatu yenye asili ya Uingereza, karibu yote yaliundwa kuwavutia waabudu wa dini mojawapo katika kundi la Maprotestanti isipokuwa koloni ya Maryland ambayo ilikusudiwa na serikali ya Uingereza kuwavutia Wakatoliki. Asili ya jina lake ni Malkia ya Scotland ambaye alikuwa Mkatoliki. Jina lake rasmi katika Kiingereza ni Mary Queen of Scots. Yeye alikatwa kichwa na ndugu yake Elizabeth, bintiye Mfalme Henry VIII. Elizabeth akawa Malkia ya Uingereza baada ya kifo cha babake.
Makoloni pamoja na mwaka wa kuasiswa yalikuwa:
1. Virginia 1607
2. Massachusetts 1630
3. New Hampshire 1623
4. Maryland 1634
5. Connecticut 1635
6. Rhode Island 1636
7. Delaware 1638
8. North Carolina 1653
9. South Carolina 1663
10. New Jersey 1664
11. New York 1664
12. Pennsylvania 1682
13. Georgia 1732
Viongozi wote wa mapinduzi ya Marekani dhidi ya Ufalme wa Uingereza walikuwa na uhusiano na makanisa ya Kiprotestanti. Wengi walikuwa waamini Mungu wasio na uanachama wa kanisa fulani. Hakuwa hata mmoja ambaye alikuwa Mkatoliki.
Lakini aliyejitenga na mkondo wa ubaguzi wa kidini alikuwa mwasisi wa koloni la Pennsylvania kwa jina anaitwa William Penn. Naye alitangaza bayana koloni la Pennsylvania inawakaribisha watu wote hata watu wa asili ya ardhi ya Marekani. Pia madhehebu ya Jamii ya Marafiki ilisisitiza usawa wa binadamu wote ijapokuwa wafuasi wake hawakuanzisha koloni yao. Ndio hao Jamii ya Marafiki ambao waliwasaidia watumwa kutoroka sehemu za utumwa na kukimbilia uhuru katika majimbo yaliyoko magharibi Marekani hadi nchi ya Kanada.
Utumwa wa Waafrika ulianza enzi za 1500 kwa vile ugunduzi wa mabara yote mawili ya Marekani na Kristo Kolombo ulitokea mnamo mwaka wa 1492. Baada ya vita baina ya Hispania pamoja na Ureno dhidi ya Uingereza, ndio Uingereza ukawa mtawala wa bahari ya Atlantiki ukawa na lengo kuwatuma walowezi Marekani ya Magharibi. Watumwa wa kwanza Marekani kutoka Uingereza walikuwa Waingereza wafungwa jela ambao waliachiliwa huru wakiwa na sharti kwenda Marekani kumfanyia kazi tajiri aliyewalipia gharama za safari. Baada ya muda unaokadiriwa kutimiza deni wakaachiliwa huru. Wengine walikufa katika joto la sehemu za kusini Marekani.
Dhamira ya makala hii ni kueleza kiini cha ubaguzi wa Waafrika Marekani ulianzia katika mgogoro wa dini baina ya Uingereza ukiwa na Kanisa la Uingereza na Kanisa Katoliki wala rangi ya ngozi ya Waafrika haikuwa na maana yoyote enzi hizo.
Ni muhimu pia kueleza rangi hiyo nyeusi ya ngozi haikuleta chuki kwa wenye rangi nyeusi. Walidanganywa kujichukia wenyewe wasije kufahamu uzuri wa rangi ya ngozi hasa kwa watu wanaofanya kazi za kishamba katika jua kali.
Chuki ya Waafrika Marekani ulianza baada ya utumwa kupigwa marufuku kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe Marekani. Kutangaza usawa wa binadamu wote kulipiga chembe na kuumiza roho za watu walioamini Waafrika walizaliwa wawe watumwa ambao hawana haki ya uraia Marekani wala uwezo kujiendeleza Marekani wala historia yoyote ya mila na desturi za kiungwana walipokuwa Afrika.
Kwa hivyo hali ya utumwa kwa Mwafrika ni baraka ya Mwenyezi Mungu.
Kumnakili Askofu mjini London wa Kanisa la Uingereza alipojibu swali la matajiri kuhusu haki ya biashara ya utumwa naye akasema: “Ukitaka kumchukia Mwafrika mwachilie adode mikononi mwa mamake huko Afrika. Kitendo hicho kitaonyesha chuki dhidi yake Mwafrika kwa vile atakuwa amekosa fursa ya kuongozwa na mwungwana.”

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s