DAKIKA 480 ZILIVYOPAGAWISHA MASHABIKI 10,000 KILIMANJARO

Profesa  Jay

Profesa J akipagawisha Kilimanjaro

Na Henry Mdimu, Mwananchi Posted  Tarehe 31 Mwezi wa Tano 2014  saa 13:35 PM

KWA UFUPI

Ikiwa ni siku ya uzinduzi, tofauti na matamasha ya miaka mingine, tamasha hilo lililofanyika Jumamosi iliyopita, lilianza na kumalizika kwa wakati kama ratiba ilivyopangwa huku wasanii wakitumia muda wa saa.

Kilimanjaro. Mji wa Moshi na vitongoji vyake mkoani Kilimanjaro ulisisimka na kutikisika, wakati mashabiki 10,000 wa muziki walipofurika kushuhudia tamasha la kwanza lililojumuisha wasanii 10 wa muziki wa kizazi kipya waliotumia dakika 480 kuburudisha katika ziara maalumu inayojulikana kwa jina la Kili Music Tour.

Ikiwa ni siku ya uzinduzi, tofauti na matamasha ya miaka mingine, tamasha hilo lililofanyika Jumamosi iliyopita, lilianza na kumalizika kwa wakati kama ratiba ilivyopangwa huku wasanii wakitumia muda wa saa.

Msanii aliyekata utepe katika uzinduzi huo alipanda jukwaani saa 4.00 asubuhi, huku wa mwisho akipanda saa 12 jioni muda ambao ulikata kiu ya mashabiki walioonekana kuridhika.

Ziara hiyo inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, ikiratibiwa na Kampuni ya EATV, East Africa Radio, Executive Solutions, Integrated Communications na AIM Group, ambayo haihusiani na washindi wa Tuzo za Muziki za Kilimanjaro, Kili Music Awards, bali inalenga kuwasaidia wasanii kuwafikia wananchi wa mikoani ili kutangaza kazi zao na kutoa burudani.

Tamasha la Moshi lililofanyika Chuo Kikuu cha Ushirika, lilikuwa la aina yake, lililojaa shangwe na msisimko kundi maarufu la Reggae mkoani Kilimanjaro, Warriors from the East ndilo lililokata utepe wa burudani ya muziki, likafuatiwa na msanii Young Killer, aliyejizolea umaarufu mkubwa siku za karibuni.

Akiwa msanii wa tatu kupanda jukwaani, Profesa Jay ambaye ni msanii mkongwe, alithibitisha kwamba kuwepo kwake ndani ya medani ya muziki wa kizazi kipya kwa muda mrefu kunaweza kuwa sababu ya msingi ya kumkusanyia mashabiki wa rika zote, hali iliyodhihirishwa na kelele za shangwe alizopata kutoka kwa mashabiki baada ya kupanda jukwaani na kutoa burudani kwa dakika 40.

Kama hiyo haitoshi, wakazi wa Moshi walizidi kupagawishwa na burudani, wakati msanii AY, naye alipotawala jukwaa kwa dakika 20 mfululizo pale alipoibuka katikati ya onyesho hilo kumsindikiza swahiba wake Mwana FA na kuibua shangwe zilizomlazimisha kuimba wimbo wake mmoja, kabla ya kumwachia Mwana FA kumalizia ngwe yake na wimbo wake mpya aliomshirikisha G Nako, unajulikana kwa jina la Mfalme.

Wakizungumza baada ya onyesho hilo, wasanii Mwana FA, Profesa Jay na Kala Jeremiah walionyesha kufurahia mapokeo ya mashabiki wa Moshi walioonyesha uchangamfu muda wote.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe, ambaye alihudhuria tamasha hilo, alisema kuwa mwaka jana Moshi iliweka rekodi ya kuwa na watu wengi zaidi na mwaka huu pia wameonyesha kuwa wanapenda burudani pamoja na kuonyesha uzalendo kwa wasanii waliotoa burudani kumshangilia kwa nguvu muda wote kila aliyepanda jukwaani.

“Moshi imeonyesha mfano mzuri, tunatumai mikoa mingine pia ikaleta msisimko kama huu, ili lengo la kuwapeleka wasanii hawa litimie. Lazima tuwakubali wasanii wetu kwanza ndiyo wakubalike nje. Kilimanjaro Premium Lager itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kupeleka muziki wa Tanzania kwenye kilele cha mafanikio,” alisema Kavishe.

Baada ya mji wa Moshi, ziara hiyo itaelekea Mwanza Mei 31, Kahama Juni 7, Kigoma Juni 14, Iringa Juni 21, Mbeya Agosti 9, Dodoma Agosti 16, Tanga Agosti 23, Mtwara Agosti 30, Dar es Salaam Septemba 6,

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s