NDOTO YANGU JUU YA MWALIMU

ef=”https://petemhunzi.files.wordpress.com/2014/06/mg_0012-8×10.jpg”>Profesa Pete M. Mhunzi
Umati wa watu ulikuwa umejaa tele barabarani. Wale wanaoandamana ndio wazee huku watazamaji ni mkusanyiko wazee kwa watoto. Barabara kuu mjini Los Angteles imevutia watu kutoka sehemu zote za mji huu kuja kusherehekea “Siku ya Wazee”.
Nilikuwa ninasimama juu juu kwenye jengo la ngazi nne kuanzia chini na kupanda
juu kila ngazi ni bao refu la kukalia na chini yake bao jingine la kupitia ambako kila mtazamaji amelisimamia apate nafasi kunasa yatokeayo kwenye wazee wanaoandamana chini barabarani.
Wazee wale wamefurahi wakisonga mbele mtindo wa wanajeshi wa jeshi la ngoma,
guu baada ya guu unapiga mdundo wakati miili ikitikisia vipigo vya wapigaji ngoma waliokuwa wanasimama katika milolongo ya pande zote mbili za barabara.
Vigelegele vikasikika. “Heko akina mama!” “Pongezi akina baba!” “Oye mabibi!”
“Oye babu zetu!” Mdundo unaodundadunda ulirusha kila mtu , mzee kwa mtazamaji.
“Du! Haiwezekani! “ Nilitazama kwa mara ya pili pale chini kwenye ngazi ya kwanza. “Macho yangu yananighilibu! Ninaota nini?” Kwa mara nyingine nikalitembeza chini jicho darubini likimlengesha mzee mpole mwembamba tabasamu ya ukarimu inamtambulisha katika sura yake. “Ni yeye!” Nikajisemesha. “Ndiye yeye!”
Mheshimiwa Rais wa Kwanza Mwalimu Julius Kambarage Nyerere! “Yuko hapa! Hapana, ni ndoto! Haiwezekani!” Naye akitazama maandamano pamoja na watu wengine pasi na hulka za maringo wala ujumbe wa walinzi wala wadau amefurahishiana na wote waliopo karibu naye. Nami nikashuka chini fastafasta kwenda kwake wasiwasi ndiyo inanikunja uso. “Shikamoo Mwalimu!” “ Marahaba! Hujambo?” “ Sijambo! Karibu kwetu Los Angeles!” “Asante!”
Mji wa Los Angeles ni mji mkubwa kushinda miji yote Marekani katika eneo. Uko
ndani ya jimbo la Kalifornya ambalo liko kwenye mwambao wa magharibi unaokabili Bahari ya Pasifiki.
Kuna miji miwili mikubwa mingine pamoja na Los Angeles katika jimbo la Kalifornya nayo ni San Francisco na San Diego. Mmoja mwingine mdogo angalau muhimu ni Sacramento ambao ni mji mkuu wa Kalifornya ambapo serikali ya jimbo pamoja na ikulu ya gavana zipo.
Lugha ya asili ya majina hayo yote ni Kihispania si Kiingereza kwa vile Kalifornya lilikuwa jimbo la Meksiko nchi ambayo ilikuwa koloni ya Hispania. Likawa jimbo la Marekani mnamo mwaka wa 1850.
Neno Kalifornya asili yake ya kimsingi ni neno “Khalifa” kutoka Kiarabu lugha ambayo iliathiri Kihispania kwa kiasi kikubwa kutokana na miaka mia tatu ya utawala wa sehemu za kusini za Hispania wa Wamori kutoka Afrika Kaskazini. “Nimeshangaa kukutana na wewe hapa Los Angeles! Imekuwaje kuja kwako isitoshe kuwepo kwenye sherehe za kuwapongeza wazee?”
“Wajua napenda Kalifornya sana kwa sababu hali ya hewa inanikumbusha na ile ya Arusha.
Nimekuja kupumzika tu halafu nikasikia habari za kumbukizi na maandamano nikaona afadhali nije kutazama wazee wa Kimarekani wanapiga guu namna gani!” “Vizuri sana!” Karibu sana!” Tukaendelea kuwatazama waandamaji wakisonga mbele katika mkondo wa udundadunda guu baada ya guu. Wapigaji ngoma nao walisowera wakitia mchakamchaka mwenendo wa waandamaji huku watazamaji wengine nao wakasakatasakata na kuninguaningua wakajizoa huko ngomani.
“Twende tukonge roho!” “Asante.” Tukaenda kwa kibanda panapopikwa chakula cha Kimeksiko. Nikamkaribisha mwalimu kinwaji msingi wake mchele jina lake “horchata”. Halafu nikaagiza taco mbili zenye nyama ya kuku, mbili zenye samaki na mbili zenye nyama choma ya ng’ombe. Aliposikia neno “taco” mwalimu alistuka kidogo nikamwambia “usiwe na wasiwasi! Ni jina la Kihispania mbali na maana yake katika Kiswahili!” Mwalimu akacheka nami nikamfuata katika uchangamfu . Msingi wa taco yenyewe ni aina ya mkate wa Kimeksiko inafanana na chapati isipokuwa ndogo, nyembamba, na rahisi. Unga wake ni wa mahindi, jina lake ni “tortilla”. (Matamshi yake ni “tor-ti-ya”) Nyama, vitunguu, nyanya, jibini na pilipili hoho zinafungwa ndani halafu!
Mwalimu alifurahia chakula kipya kwake. Baada ya shibe tukaanza kutembea tukitazama vitu vilivyopambwa kwenye vibanda rangirangi zinang’aa zikishika macho ya wanaopitapita. Vingine vilikuwa vya Kiafrika hata kanga, bangili za fedha na dhahabu, hereni za kuning’inia pamoja na batik, mikanda na kundavi zilimrudisha Mwalimu mtoni.
“Mwalimu! Shikamoo!! Sauti ilisikika ndani ya kibanda kimoja chenye vitu vya Tanzania. Tukamwona mwanamke mmoja tabasamu ya nuru macho yanashangaa ndani ya sura ya uchangamfu. “Marahaba! Hujambo? Mambo?” “Mambo poa kabisa!” Naye aliitikia akizidi kuamini pamoja na kuduwaa akitoka kibandani kutujia.

“Walahi! Ya Mungu ni mengi! Sijui ninaota au mazingaombwe! Ni kweli! Mwalimu wetu yupo mbele yangu papa hapa Marekani!” “Ndiyo Bi. Mdogo ni mimi! Nimefurahi sana kuonana nawe jina lako nani?” “Jina langu ni Rehema Mwanahuria kutoka Buguruni Darsalama mzaliwa Dodoma “.
“Ala! Mgogo ‘we!” “Hapana mimi ni Mnubii” “Basi haidhuru! Sisi sote Watanzania! Hebu, unauza nini hapa?” Bi. Rehema aligeuka kurudi kwenye kibanda kanzu aliyoivaa rangi ya waridi ikishikamana na mwendo wake wa maringo. Mrefu si mwembamba si mnono mfano wa siha umbo wa kuumbika mlimbwende mwenye kulijaza neno hilo maanani. Tukamfuata hadi meza ya mbele. Kanga za kila rangi zimepambwa juu yake katika safu tatu huku katikati ya safu bangili zimekaa zikimetameta na kumulikia zaidi rangi za khanga zote kuwa pamoja katika taswira ya bustani yenye kila aina ya maua. Mwalimu alipendezwa akatazamatazama hana la kusema. “Subiri kidogo! Nikuletee kitu adimu sana!” Bi. Rehema akaelekea meza ya nyuma chini yake akafungua sanduku kubwa akatoa kinyago. “Sasa!” Alitukabidhi kinyago cha mpigaji ngoma anayepiga ngoma kumi na mbili. Hapana ila Mzee Morisi!
Sura ya mwalimu ukawaka ukamulika nuru iliyomrudisha utotoni ngozi laini haijapaswa kukunjika. Akacheka kicheko sauti yake inatokea moyoni ikisikika kama ndege mitini wanaoimba uhuru wa roho shukran za maisha. Hawana woga, hakuna shida ni maisha ya ahadi. Tukatazamana mimi na Mwalimu tukashukuriana. Nami nikaingia usingizi mnono. Ndoto imesharudi moyoni mwangu hata akili sasa imepata utulivu na kuhifadhiwa hadi niwe macho.
na Pete M. Mhunzi
27 Mwezi wa Nane 2013

Advertisements

One thought on “NDOTO YANGU JUU YA MWALIMU

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s