FASIHI YA KISWAHILI IKITUMIKA VYEMA, KWA WAKATI, ITASAIDIA KUJENGA MAADILI

Gadi Solomon

MWANANCHI, Tarehe 10 Mwezi wa Kumi na Mbili, 2012

Fasihi ya Kiswahili ikitumika vyema, kwa wakati, itasaidia kujenga maadili

Na Gadi Solomon

KWA UFUPI
FASIHI ya Kiswahili kupitia matawi yake ya fasihi simulizi na fasihi andishi yana nguvu ya kuleta mabadiliko katika jamii iwapo yakitumika ipasavyo na kwa wakati.

FASIHI ya Kiswahili kupitia matawi yake ya fasihi simulizi na fasihi andishi yana nguvu ya kuleta mabadiliko katika jamii iwapo yakitumika ipasavyo na kwa wakati.
Kupitia fasihi andishi katika riwaya na mashairi tanzu, hizo zimekuwa mwiba kwa watu wenye mwenendo mbaya katika nafasi zao za uongozi na hata katika jamii.

Fasihi kwa kawaida imekuwa ikigusa maisha halisi ya wanajamii kwa kuonyesha mambo mbalimbali kama vile athari za ulevi, wivu katika mapenzi ushirikiana,fitina na chuki jinsi zinavyorudisha nyuma gurudumu la maendeleo katika jamii.

Kupitia fasihi ya Kiswahili, waandishi wengi hawakuwa nyuma kuonya athari za vita na kuifanya jamii yetu kutunza tunu ya amani tuliyonayo licha ya kasoro zinazojitokeza hivi karibuni kutokana mitazamo tofauti ya watu wachache.

Mara nyingi waandishi wa vitabu katika kuwasilisha kile alichokusudia, anaweza kutumia taswira mbalimbali ili kumfikirisha msomaji.
Mfano itakumbukwa katika vitabu mbalimbali vya riwaya na mashairi mfano wa taswira zinazoashiria jambo fulani, kama vile; kupe, samaki, dagaa,unga, njiwa huku wakibebesha dhamira tofauti ili kufikisha ujumbe kwa jamii husika.
Hata hivyo itakumbukwa kila mtu anaweza kutumia sanaa katika kukemea jambo baya katika jamii.
Yapo mambo mengi ya kujiuliza bado ipo haja ya kufikisha jambo kwa kufichaficha ili kukidhi matakwa ya wadhamini ambao mara nyingi hupenda mambo kuwekwa kwa kificho ama wasikosolewe.

Mathalan, waandishi na watunzi wa vitabu hivi karibuni wamejiona matukio mbalimbali yanayotokea katika jamii yetu yanayotakiwa wapaze sauti zao kupitia fasihi ya Kiswahili, na yanapaswa kusemwa waziwazi ili kuwafunza jamii ya vijana na watoto mambo mema wanayopaswa kufuata.

Miongoni mwa mambo ya msingi ya kuyaweka wazi jamii inapaswa kuelezwa kwa kina zaidi kuhusu uwapo chama kikuu cha upinzani.

Wanachama wa vyama hivyo yamkini wakawa na uelewa wa mambo yanayohusiana na siasa, lakini kwa upande mwingine watunzi wa sasa wanapaswa kutoa elimu hiyo kwa jamii kwa jumla ili watambue siasa haina maana ya chuki miongoni mwa wanajamii.
Haina haja ya kutumia taswira za kuficha ficha jambo kama hilo kutokana na ukweli kwamba hata watu wa kawaida wanapaswa kusoma maarifa hayo ili yawasaidie.
Hapa nchini kwa bahati mbaya utanzu wa wimbo umekwenda mbali zaidi na kugeukia maudhui ya wa mapenzi kwa kiasi kikubwa.
Hata hivyo, utanzu huo nao unaweza kuwa chachu ya kukemea rushwa na ufisadi katika jamii mambo ambayo yameonekana kujitokeza kwa asiliamia kubwa miaka ya hivi karibuni.
Tuna vitabu vingi vya fasihi ambavyo vinatumika katika shule ya msingi na sekondari pia vyuoni, lakini mambo hayo ambayo yamekuwa yakifundishwa.
Pia, vijana wanapomaliza kidato cha nne huusiwa kufuata yale ambayo wameyapata kutoka vitabuni na kutoka kwa walimu wao, sasa inaonekana ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.
Vilevile, hayo yanayokatazwa, ndiyo yamekuwa yakitokea katika jamii zetu. Mfano mimba za utotoni, unyanyasaji wa kijinsia, rushwa na ujfisadi.

Fasihi ya Kiswahili imefanya kazi kwa nafasi yake na watunzi kujitoa kwa kuandika maudhui yanayoizunguka jamii ili kuweza kuielimisha.
Vitabu vya fasihi sasa katika shule za sekondari, vinapaswa vionyeshe nafasi ya kila mwananchi katika ushiriki wake katika kujiletea maendeleo na kushiriki ili kunufaika na soko la ushindani.
Vitabu vya sasa visikwepe kueleza athari za mauwaji ya albino kwa taifa, jambo ambalo ni dhana potofu ambazo zimekuwa zikishikiliwa na baadhi ya watu wanaoamini kupitia viungo vya albino vinaweza kuwapitia utajiri.
Fasihi ya Kiswahili ya leo ieleze umuhimu wa wananchi kulipa kodi kwa Serikali yao iwapo wanayatamani maendeleo na huduma bora ikiwa ni pamoja na kudai risiti pindi anaponunua bidhaa.
Fasihi ya sasa ihamasishe vijana kujiajiri kuliko kuwa walalamikaji kila kukicha ili kujipatia kipato. Hiyo ni pamoja na kubuni njia ya kupata kipato cha ziada hata kama anapata mshahara.
Vilevile fasihi ya sasa iwakumbushe vijana kuhusu umuhimu wa kujali afya zao ikiwa ni pamoaja na kuacha kutumia vyakula vya kemikali, kutumia dawa za kuongeza maumbo ya miili yao. Kwani hii ni hatari kwa nguvu kazi ya taifa.
Bila kuficha fasishi ya sasa ionyeshe njia ya vijana kupambana na tatizo la ajira ikiwa ni pamoja na kujiunga na vikundi vya ujasiriamali na kuondokana na tabia ya kushinda katika vikundi jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa maisha yao.
Fasishi ya sasa ieleze mabadiliko ya tabianchi na kuifanya jamii kuwa sehemu ya kutunza mazingira ili kuepukana na ukataji miti ovyo. Siyo kusubiri mpaka siku ya mazingira ndiyo tusikie umuhimu wa jamii kushiriki katika kutunza mazingira.
Fasihi ya sasa iwakumbushe vijana kuepukana na migomo sehemu ya vyuo na shuleni bila kufuata utaratibu jambo ambalo mara kadhaa imewasababishia wengi wao kufukuzwa ama hata kuharibu ndoto za maisha yao baada ya kukosa nafasi ya kuendelea.

Huko vyuoni fasihi ya sasa ionyeshe namna ya kukabiliana na mazingira ya vyuoni na kuepuka makundi yanayojihusisha na uuzaji miili yao ili kujipatia fedha za kujikimu kama ilivyoripotiwa katika vyombo vya habari wiki chache zilizopita na katika mitandao ya kijamii.
Ni vyema pia mfumo wa shule zetu sekondari na shule ya msingi wakaweka utaratibu kila mwanafunzi lazima awe amesoma vitabu vya kiada na ziada kadhaa, ili kuweza kuwa na jamii yenye uelewa wa mambo mbalimbali.

 

Advertisements

One thought on “FASIHI YA KISWAHILI IKITUMIKA VYEMA, KWA WAKATI, ITASAIDIA KUJENGA MAADILI

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s