TV, REDIO ZIFUNDISHE KISWAHILI WATANGAZAJI WAO

Stephen Maina

Na Stephen Maina

MWANANCHI Tarehe 22, Mwezi wa Sita 2014
KWA UFUPI
Mifano hii michache inaonyesha jinsi tunavyoidhalilisha lugha yetu. Pamoja na hayo liko kundi jingine ambalo lina sauti kubwa katika jamii.

Nimewahi kuandika kuwa kuchanganya Kiswahili na Kiingereza katika kuandika habari makala au katika mazungumzo rasmi ni kukidhalilisha Kiswahili.
Waandishi na wazungumzaji wa aina hii hawako makini na hawajali kuzingatia ufasaha wa Kiswahili.
Nilieleza kidogo katika makala zangu zilizopita kwamba watangazaji hasa wa redio na runinga zilizosajiliwa katika miaka ya hivi karibuni ndizo zisizotilia mkazo mafunzo ya lugha kwa wafanyakazi wao ili kuwainua kitaaluma kwa kuwaandalia semina na warsha za kuboresha taaluma yao katika fani za uandishi na utangazaji.
Nitatoa mifano michache ya makosa yanayofanywa na watangazaji wa runinga na redio. Kwa mfano utawasikia watangazaji wakisema:
Message unazopeleka ni za nani?
I remember kwenye semina ya ndoa mambo yalikuwa safi.
Lakini a good office is well arranged
Hiyo infrastructure ni mbovu.
Lazima ufokasi kwenye future na maelezo mengine mengi.
Mifano hii michache inaonyesha jinsi tunavyoidhalilisha lugha yetu. Pamoja na hayo liko kundi jingine ambalo lina sauti kubwa katika jamii.
Kundi hili ni la wanasiasa na hasa wabunge ambao wanapojadili hoja bungeni au wanapowahutubia wananchi, jamii nzima ya Watanzania kukaa macho kufuatilia kinachozungumzwa.
Wako baadhi ya wanasiasa wanapozungumza hawako makini katika uchaguzi wa misamiati au istilahi za kutumia.
Kwa kuwa muda wa kuzungumza ni mfupi, kiwazo wanachokabiliana nacho ni uchaguzi wa maneno.
Ufahamu wa lugha mbili ambazo zimekubalika bungeni umewafanya wabunge wachanganye lugha.
Ninavyofahamu ni kuwa kama uliamua kutumia Kiswahili basi tumia Kiswahili moja kwa moja. Kama unataka kutumia Kiingereza basi tumia Kiingereza moja kwa moja ili wanaofahamu Kiingereza nao wafaidi.
Ila kuchanganya lugha hizi mbili kwa pamoja katika mazungumzo unawakosea haki baadhi ya wasikilizaji wako.
Swali la kujiuliza ni kwa nini wanasiasa na watangazaji wa siku hizi hawana umakini katika matumizi ya lugha fasaha na iliyo sanifu wanapowatangazia Watanzania na dunia kwa jumla?
Ijapokuwa sijafanya utafiti wa kina lakini kwa uzoefu wangu wa miaka mingi katika fani hii ya matumizi ya Kiswahili katika shule na vyuo, nimegundua kuwa vijana wengi wanataka kujifanya kuwa ni wasomi hata kama amefikia kidato cha nne au sita.
Ukweli ni kuwa kama una elimu ya sekondari na hata ya chuo kikuu bado huna haki ya kujigamba kuwa ni wewe ni msomi. Inashauriwa kuwa kujielimisha ni wajibu wetu sote kwani hatuko wakamilifu.
Sifa mojawapo ya kuwa msomi ni kuzungumza lugha inayoeleweka kwa jamii nzima ya Watanzania.
Nimewasema watangazaji katika vyombo vyetu vya habari pamoja na wanasiasa, lakini ingekuwa bora zaidi na kwa ajili ya manufaa ya umma kama Serikali ingekuwa na sera ya lugha inayotakiwa kufuatiliwa kwa makini.
Nafahamu kuwa Serikali imeunda chombo tangu mwaka 1976 cha kusimamia na kuratibu lugha ya Kiswahili Tanzania lakini hakina meno. Ina maana ya kuwa na sheria itakayowafanya viongozi, waandishi na watangazaji kuwajibishwa kama vile kupewa maonyo endapo watakapokiuka maadili ya lugha.
Nimewasema wanasiasa, waandishi na watangazaji pamoja na Serikali kila moja kutimiza wajibu wake. Hata hivyo, ieleweke kuwa hayupo mtu au chombo cha kunyooshewa kidole.
Wote tuna wajibu wa kuona kuwa tunaithamini lugha yetu na huo ndiyo uzalendo tunaoupigania.

stephenjmaina yahoo.com

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s